Masharti ya huduma
Free hutolewa mara moja kwa akaunti: maswali 5, picha 1 na video moja ya sekunde 5, kwa nafasi 10 za kwanza za majaribio. Usifungue akaunti nyingi kukwepa kikomo.
Anza ni $2 kwa siku 30: maswali 100 na picha 5. Lite ni $5 kwa siku 30: maswali 200, picha 15, video 1 ya sekunde 5 na uchambuzi wa kina 2.
Credit za matumizi hununuliwa kabla ya kazi: maswali 20 ni $0.50, picha 1 ni $0.15, video 1 ya sekunde 5 ni $0.90 na uchambuzi wa kina 1 ni $1. Bei ya TSh inayoonyeshwa kabla ya kulipa ndiyo inayotumika. Haya si makato ya kiotomatiki baada ya ombi. Credit za matumizi zinaweza kununuliwa bila kifurushi, hazifuti kifurushi kilichopo na hazijawekewa mwisho wa muda katika toleo hili; hupungua zikitumika. Credit za kifurushi au Free hutumika kwanza, kisha credit za matumizi za huduma hiyo. Kubadilisha au kuisha kwa kifurushi hakufuti credit za matumizi zilizobaki.
Pro ni $12 kwa siku 30. Plus $20 na Creator $50 ni za siku 30. Vifurushi vya $100, $200, $300 na $400 ni vya siku 365; credit zake ni za mwaka mzima, hazijirudishi kila mwezi. Jedwali la vifurushi kwenye Studio linaonyesha idadi ya maswali, picha, video na uchambuzi wa kina kwa kila kipindi.
Huduma husimama credit za aina hiyo zikiisha; credit zote zikiisha kifurushi hakiwezi kutoa huduma nyingine bila ununuzi mpya. Credit za kifurushi zilizobaki huisha mwisho wa kipindi. Hakuna malipo ya kujirudia yenyewe, wala kuhamisha credit za kifurushi. Credit za matumizi hubaki kando. Kifurushi kipya huanza fedha zinapothibitishwa na kinachukua nafasi ya kilichopo mara moja, bila kuhamisha credit za zamani. Hali hii inaonyeshwa kabla ya kutuma ombi la malipo. Bei ya mwisho ya TSh inayoonyeshwa kabla ya kulipa ndiyo inayotumika; usilipe kama bei haijawekwa au malipo hayajafunguliwa.
Uchambuzi wa kina hutumia modeli ya reasoning na taarifa unazotuma. Kiwango cha kifurushi huongeza kiasi cha matumizi na urefu wa taarifa; hakitoi dhamana ya usahihi, ruhusa ya kitaalamu, wala utafiti wa mtandaoni. Hakiki hitimisho na hesabu dhidi ya vyanzo vinavyoaminika.
AI inaweza kukosea. Hakiki matokeo, haki za matumizi, matamshi na mwendo wa midomo kabla ya kuchapisha. Hatuhakikishi lafudhi, uhalisia kamili au kutimiza kila ombi. Tumia picha, sauti na maandishi unayoruhusiwa kutumia; usitumie huduma kwa ulaghai au kuiga mtu kwa udanganyifu.
Ombi lililokataliwa wazi na mtoa modeli hurejeshewa credit ya ndani. Kazi iliyotumwa na kukatizwa bila matokeo yanayojulikana inaweza kubaki inasubiri ukaguzi ili kuzuia matumizi mara mbili. Ukiwa na tatizo wasiliana na 0749488769 ukiwa na kitambulisho cha kazi; usitume key, PIN au OTP. Malipo yaliyothibitishwa kuwa ya kurudia au ya huduma isiyowasilishwa yatakaguliwa na mwenye huduma kwa marejesho yanayostahili.
Ramani hutegemea Geoapify/OpenStreetMap na maeneo yaliyorekodiwa. Umbali wa mstari wa moja kwa moja si umbali wa barabara. Muda wa safari ni makadirio, si taarifa ya msongamano wa moja kwa moja. Uongozaji hai hufunguliwa Google Maps kwa ruhusa na upatikanaji wa huduma yake. Hatuhakikishi kila eneo, barabara au hali ya njia; kagua alama na hali ya eneo.
Usitume pesa wakati ukurasa unasema malipo hayajafunguliwa. Huduma hutegemea upatikanaji na salio la watoa modeli. Akaunti inaweza kusimamishwa kwa matumizi mabaya.